Watu watatu wamefariki papo hapo huku wengine wawili wakilazwa katika hospitali kufuatia ajali ya barabarani katika barabara ya Tawa- Mbumbuni eneo la Katithi Mbooni Mashariki Makueni asubuhi hii. Akithibitisha hayo kamanda wa polisi kaunti ya Makueni Joseph Ole Napeiyan amesema ajali hiyo imehusisha pikipiki mbili ambazo zimegongana ana kwa ana. Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Tawa majeruhi wakilazwa katika hospitali iyo hiyo. Polisi wanaendesha uchunguzi zaidi.