Home Uncategorized ‘Uhuru ameshindwa kuitawala Kenya’, adai Mbunge Oscar Sudi

‘Uhuru ameshindwa kuitawala Kenya’, adai Mbunge Oscar Sudi

1091
0

NAIROBI, KENYA, Jinsi ilivyotarajiwa Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ambaye ni mwandani wa Naibu wa Rais William Ruto amejitokeza kulalamikia hatua za hivi punde za kufunguliwa mashtaka kwa Waziri wa Fedha Henry Rotich miongoni mwa maafisa wengine wakuu serikalini.

Mbunge huyo amerejelea kauli ya awali ya Ruto kwamba hakuna fedha zilizoibwa katika miradi ya mabwawa ya Arror na Kimwarer akisisitiza madai hayo yaliibuliwa na watu wenye njama ya kusambaratisha utekelezaji wake.


Wakati wa kikao na wanahabari mjini Eldoret, Sudi amesema kwasasa taifa hili linakabiliwa na mgogoro wa uongozi ambao umechangiwa na ushirikiano baina ya Rais Kenyatta na kinara wa ODM Raia Odinga

Kwa kuzingatia hayo yote, mbunge huyo amekata kauli Rais Kenyatta ameshindwa kuangazia changamoto zinazoshuhudiwa nchini ikiwamo mvutano kuhusu mgao wa fedha za  kaunti na mgogoro baina ya viongozi katika Chama cha Jubilee. Kadhalika amedai ana uwezo zaidi wa kuongoza taifa kumshinda Kenyatta na Ruto huku akimpendekeza Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria kuwa naibu wake.

Hata hivyo katika ujumbe katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Kuria amempuuza Sudi  akimtaka akome kumhusisha na masuala yaliyoko mahakamani.  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here