NJIA MWAFAKA ZA KUACHANA NA MPENZI WAKO
Mdau wetu ameainisha njia zifuatazo kuwasaidia wadau kumaliza mahusiano na wenzi wao kwa amani
1. Kuwa na Uhakika na unachotaka kufanya: Kama huna uhakika juu ya hisia
zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo
maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi thabiti
2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano: Unapojua sababu zinazopelekea
wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale
unapoulizwa
3. Maliza Mahusiano wewe Binafsi: Kama umekuwa na mpenzi wako kwa muda
mrefu au kipindi chochote, uliwekeza muda na nguvu zako za kujenga
mapenzi, hivyo ni busara mahusiano hayo ukayamaliza mwenyewe
4. Msikilize mwenzi wako: Hata kama umeshaamua na huwezi kubadili mawazo
juu ya kuvunja mahusiano yenu, haina maana kuwa usimsikilize mwenzi
wako
5. Kuwa Mtulivu na Makini: Unahitaji kuumaliza uhusiano na kuondoka mahali mlipo. Hata hivyo, ni busara kuwa mtaratibu na mpole
Je, nini uzoefu wako kuhusu kuacha au kuachwa katika mahusiano?