Home Uncategorized Kenya kuagiza mahindi kutoka Tanzania

Kenya kuagiza mahindi kutoka Tanzania

600
0

Akizungumza wakati wa kupokea kilo 35 za dhahabu iliyokuwa imeibwa kutoka nchini humo, Rais wa Tanzania John Magufuli amedokeza kwamba mkataba wa kuizuia Kenya mahindi ni miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa wakati wa ziara ya Rais Kenyatta nyumbani wake hivi karibuni.

Wakati wa kupokea mzigo huo, Rais Magufuli alifanya mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Kenyatta kupitia simu.

Waziri wa Masuala ya Kigeni Monicah Juma, Mkuu wa Mashtaka Noordin Hajj, Mkuu wa Upelelezi George Kinoti na Katibu wa Kilimo Hamadi Mboga ni miongoni mwa waliousindikiza mzigo huo uliobebwa na ndege ya kijeshi. Baadhi ya maafisa hao  wanatarajiwa  kuendeleza mazungumzo kuhusu mkataba  huo wa mahindi na masuala mengine.

Kwa mujibu wa Katibu  wa Kilimo, Hamadi Mboga  licha ya wakulima wa eneo la Bonde la Ufa kulalamikia hatua ya kuagizwa mahindi kutoka nje ya nchi, kuna upungufu mkiubwa wa bidhaa hiyo kutokana na kuchelewa kwa msimu wa mvua mwaka huu.

Kwa mujibu wake, Kenya inahitaji mahindi katika magunia zaidi ya milioni 4.3 kila mwezi. Kuanzia mwezi uliopita, baadhi ya wasagaji mahindi wamelazimika kusiyisha shughuli zao kwa kukosa mahindi.

Ikumbukwe, wakulima wa mahindi katika Bonde la Ufa  wamekuwa wakipinga mpango wa kununua mahindi katika magunia zaidi ya milioni 12.5 huku wakisistiza  kwamba serikali iweke wazi kiwango cha upungufu na kuhakikisha mahindi yananunuliwa kwanza kabla ya shughuli hiyo kuelekezwa nje ya nchi.

READ

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here