Uncategorized

Gor Mahia yamnyemelea nyota wa Sofapaka na Harambee Stars

Mabingwa mara 18 wa ligi kuu nchini Gor Mahia, wameingia katika vita vikali vya kunasa huduma za nyota wa Sofapaka John Avire.

Kocha wa Kogallo Hassan Oktay amedhibitisha penzi lake kwa mchanaji huyo wa Harambee Stars,akifichua kwamba amejaribu kumsajili kabla ya kuelekea Misri.

Oktay amesisitiza kwamba anahitaji mshambuliaje mwenye uzoefu ili kupiga jeki juhudi zake katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

“Mashindano ya bara ni mashindano tofauti na yanahitaji ubora wa wachezaji.Nimejaribu kutafta mchezaji wa kufunga magoli ila kila ninapotaja,anasajiliwa na timu nyingine.

Nimejaribu kumsajili Avire ila nimepata habari kuwa ameelekea Misri.Avire ni mchezaji mzuri na endapo atarejea Kenya bado ntajaribu kumshawishi kwa sababu nataka kuboresha viwango vyake,”ameeleza Oktay.

Hata hivyo Avire mwenye umri wa miaka 22,ana mkataba na Batoto Ba Mungu hadi Disemba mwaka huu na amekisiwa kuwa mawindoni Misri,safari ambayo imevuruga amani katika shikisho la mpira wa miguu nchini FKF.

Juhudi za Gor Mahia za kupata huduma za mshambuliaji Derric Otanga kutoka Sony Sugar ziligonga mwamba baada ya mchezaji huyo kuamua kuingia zizini mwa mabwenyenye Wazito FC.

Gor Mahia inakabiliwa na shinikizo la kujaza mapengo makubwa yaliyoachwa na mnyarwanda Jacques Tuyisenge aliyepata mnofu nchini Angola na klabu ya Petro Atletico na Francis Kahata ambaye yuko Dar Es Salam Tanzania kupigia wekundu wa msimbazi Simba SC.

Show More

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button